Tuesday, February 21, 2012

WENYEWE HATUWEZI?

Kuondoka kwa SIDA, HIVOS na Mashirika mengine ya wazungu ambayo yalikuwa yakifadhili shughuli za sanaa katika nchi yetu imekuwa ni pigo kubwa sana kwa sanaa yetu. Vikundi na Taasisi nyingi zimefifia na nyingine kufa. Tazama Mfuko wa Utamaduni, TzTC na UWAVITA-Hii ni mifano hai na Serikali yetu haisaidii Taasisi hizi kwa lolote. Hivi Sweden, Denmark, Uholanzi au Marekani  na wengineo, nani hasa anatakiwa kuinua Sanaa hapa Tanzania? Wasanii wanajitahidi na kazi zao zinaonekana-Kwa nini Serikali haithamini jasho lao? Kwa nini haiwasapoti? Hivi kweli nchi yetu haiwezi kukuza Utamaduni wetu zaidi ya kusubiri Misaada kutoka kwa Wazungu?

Tuesday, December 27, 2011

SAMAHANI KWA USUMBUFU

KWAKO MGENI ULIYEKUWA UKIITEMBELEA BLOGU HII. SIKUWEZA KUTIA CHOCHOTE HUMU KWA ZAIDI YA MWAKA MZIMA SASA KUTOKANA NA SABABU AMBAZO HAZIKUWEZA KUZUILIKA. SASA NINARUDI TENA NA MUDA MFUPI UJAO (TUKIJAALIWA TAREHE 01.01.2012) UTAWEZA KUIONA BLOGU YAKO KATIKA MAMBO MAPYA KABISA.
ASANTE KWA KUNIVUMILIA NA KILA LA KHERI!

Wednesday, October 27, 2010

UCHAGUZI MLANGONI!

KAMA ILIVYO KWA WATANZANIA WENGINE, WASANII PIA WANA HAKI YA KUPIGA KURA. SANAA INATUWEZESHA KUJUA AHADI HEWA NA ZILE ZINAZOTEKELEZEKA.

MSANII KUWA MACHO SIKU HIYO

HAKIKISHA HUCHAGUI PUMBA!
KUWA TAYARI OCTOBER 31, 2010